Skip to content

NABU nchini Kenya

NABU ni programu ya kusoma inayopatikana kwenye simu za mikono na kwenye tableti.

Kuvipata vitabu hivi hauhitaji mtandao wenye kasi ya juu au kifaa chenye utendaji kazi wa juu bali tu hamu ya kujifunza kusoma hadithi na watoto.Lengo letu ni kuleta umuhimu na uwezo wa vitabu katika maisha ya watoto kila mahali na kujenga njia zinazofikiwa haraka za maarifa; uwezo mkubwa tunaouamini.

Pakua programu

NABU kwa watoto

Katika programu ya NABU, Utapata hadithi za kusisimua kuhusu ujasiri na urafiki tukielewa kuwa unaweza kusoma wakati wowote upatapo muda hasa wakati wa mapumziko.Wahusika wetu wanakukaribisha kwenye programu kwa kiwango chochote cha usomaji wako, kwa hadithi zinazokufundisha zaidi kuhusu ulimwengu unaoishi na jinsi unavyoweza kuufanya kuwa bora kidogo.
Tambua ni umbali gani unaweza kuenda na uanze kupenda kujifunza kusoma hata kama ni kwa dakika chache tu kila siku.
Programu yenyewe hailipiwi, hivyo waambie wazazi kuhusu NABU na ugundue unavyoweza kuundelea kwa kusoma robo ya hadithi kila siku.

NABU kwa wazazi

Tunafahamu kuwa inaweza kuwa changamoto kuwahimiza watoto wenu kusoma na kupenda kujifunza. Hata hivyo, hapa ndipo NABU inaweza saidia!, Programu hii imeundwa ili kuwawezesha kupata angalau dakika chache za kusoma kwa urahisi katika maisha yenu.


Mtoto wako anaweza kujisomea mwenyewe, unaweza kuvichagua na kuvihifadhi vitabu ili mvisome pamoja baadaye, na uendelee kuvichagua vitabu vyenye hadithi changamano kadri stadi za kusoma za mtoto wako zinapoimarika. Jambo la muhimu ni kuweza kufurahia wakati mnapokuwa pamoja. Pata programu hii bila malipo na uwape watoto nafasi ya kugundua furaha ya kusoma.

Pakua programu

NABU Kwa walimu

Tumia NABU darasani au uwaambie wanafunzi wako kuhusu programu ya NABU na uwahimize kufanya mazoezi nyumbani!

Programu ya NABU inawawezesha watoto kuchagua hadithi kulingana na kiwango chao cha usomaji, kugundua mada za kisasa katika yale wanayoyasoma na  vile vile kujifunza Kingereza/Kiswahili: Vitabu vingi vimeandikwa kwa lugha mbili. Kimsingi, wanaendeleza nyumbani unachowafundisha shuleni katika robo saa tu, kwa siku.

PaKUA programu

Kuwepo kwa NABU nchini Kenya ni mpango wa

Jisajili uwe bingwa wa kusoma na kuandika wa NABU

Jisajili hapa

squiggles
African kid smiling

Donate

Your donation makes a difference. Join us in our mission to ensure every child has equal access to literacy and learning resources.

THE IMPACT OF YOUR GIFT

NABU is free for children, families, and teachers, thanks to our generous donors. Your donation can make a big difference:

  • $25 monthly subscription for one child: Provide access to the NABU app and hundreds of bilingual books for a child and their family
  • $45 monthly subscription for one classroom: Gift NABU to a teacher for use in their classrooms to support student learning
  • $1,500 to publish a children's book: Support our professional development initiatives, training local artists to create culturally relevant stories for children in their communities, with translations into 25 languages
  • $5,000 to sponsor a country-wide children's radio program:Expand our impact through storytelling radio programs across an entire country
Donate Now

110 E 25th St.
New York, NY 10010

info@nabu.org
BadgeBadgeBadge
© 2025 Copyright - NABU (NABU GLOBAL INC) is a 501c3 non profit organization EIN: 90- 0888570.
  • Privacy
  • Terms & Conditions